Genesis 17

Agano La Tohara

1 aAbramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, Bwana akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu;
Mwenyezi Mungu hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).
enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu.
2 cNami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.”

3 dAbramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, 4 e“Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. 5 fJina lako hutaitwa tena Abramu, bali jina lako litakuwa Ibrahimu,
Ibrahimu maana yake Baba wa watu wengi.
kwa maana nimekufanya wewe baba wa mataifa mengi.
6 hNitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako. 7 iNitalithibitisha Agano langu kama Agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo niwe Mungu wako na Mungu wa wazao wako. 8 jNchi yote ya Kanaani, unakoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na uzao wako, nami nitakuwa Mungu wao.”

9 kNdipo Mungu akamwambia Ibrahimu, “Kwa upande wako, lazima ushike Agano langu, wewe na wazao wako kwa ajili ya vizazi vijavyo. 10 lHili ni Agano langu na wewe pamoja na wazao wako baada yako, Agano mtakalolishika: Kila mwanaume miongoni mwenu atatahiriwa. 11 mMtafanyiwa tohara na hii itakuwa ni alama ya Agano kati yangu na ninyi. 12 nKwa vizazi vijavyo, kila mwanaume miongoni mwenu mwenye siku nane ni lazima atahiriwe, pamoja na watakaozaliwa nyumbani mwako au walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, wale ambao sio watoto wako. 13 oAwe amezaliwa nyumbani mwako au amenunuliwa kwa fedha yako, ni lazima watahiriwe. Agano langu katika mwili wako litakuwa ni Agano la milele. 14 pKila mwanaume asiyetahiriwa, ambaye hajapata tohara ya mwilini, atatengwa na watu wake, amelivunja Agano langu.”

15 qPia Bwana akamwambia Ibrahimu, “Kwa upande wa Sarai mkeo, hutamwita tena Sarai bali jina lake litakuwa Sara. 16 rNitambariki na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki na kwamba atakuwa mama wa mataifa, wafalme wa mataifa watatoka kwake.”

17 sIbrahimu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?” 18 tIbrahimu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!”

19 uNdipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaka.
Isaka maana yake Kucheka.
Nitalithibitisha Agano langu naye kama Agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake.
20 wKwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa. 21 xLakini Agano langu nitalithibitisha kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia mwaka ujao majira kama haya.” 22 yWakati alipomaliza kuzungumza na Ibrahimu, Mungu akapanda juu akaondoka kwa Ibrahimu.

23 zSiku ile ile, Ibrahimu akamchukua Ishmaeli mwanawe na wote waliozaliwa nyumbani mwake pamoja na walionunuliwa kwa fedha zake, kila mwanaume wa nyumbani mwake, akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza. 24 aaIbrahimu alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa, 25 abnaye Ishmaeli mwanawe alitahiriwa akiwa na umri wa miaka kumi na mitatu. 26Ibrahimu na Ishmaeli mwanawe walitahiriwa siku ile ile, 27 acKila mwanaume nyumbani mwa Ibrahimu, pamoja na wote waliozaliwa nyumbani mwake au aliyenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, alitahiriwa pamoja naye.
Copyright information for SwhKC